Sun 09 Dec, 2018 22:15:42 EAT
652 Views |
0 Comments |
68 Likes
Akhera Yamngoja
Kuzaa si kazi,kulea ndiko.
Meno kaota ,matendeguu anazo.
Kaptura kafuma,kutambaa kaaga.
Kupakatwa kwaisha, akhera yamngojaa.
Mtoto umleavyo,ndivo akuavoo.
Nepi katupwa ,ndio pamper zitumukee,
Yaya kashughulika , mamake mitandao aiingiee.
Kupakatwa kwaisha,akhera yamngojaa.
Matundakamea,janajikekatokea.
Shule kapitiaa,masomo kahitimia.
Shahada katunukiwa,ulimwengu kamkaribisha.
Kupakatwa kwaisha,akhera yamngojaa.
Wanja kwa hinaa,mwanamwali katokomea,
Mapambo kwa mapambaa,tako lonekanaa.
Miti kwenye mitaa, afya kadororaa.
Kupakatwa kwaisha, akhera yamngoja
©Expired Giant
Prev : On My Way To Canaan Next : I Had To Do It