Kauli


kechi kenyatta / expired giant

Kauli

By kechi kenyatta / expired giant

Mon 06 Mar, 2017 23:29:09 EAT
820 Views | 10 Comments | 84 Likes

#penzi  #uamizi  


Kauli

Anapocheza lelema
Ananifanya nileuke mwishowe naleleja
Umbo lake mviringo
Kiuno chake lembelembe
Hayo yote yanichanganya
Msimamo wangu huwa thabiti
Na tayari umegeuzwa kuwa legelege
Sio eti Mimi mlevi
Ila mwenzenu amerogwa na penzi.

Nina kanionya kumhusu,
Lakini naona nikikaidi.
Maana mtoto yule kaiva,
Rangi yake rajamu.


Rasilimali kwangu rasimu
Japo ramli ninayo
Ila si mwitaji rasuli
Ndipo ndoa yetu raufu

Heri niwe mtumwa
Na.nikubali utobwe
Na nihepe shadidi,
Maana upweke waeza niua,
Heri nifuate penyo.
Licha ya kuwa upeo.
Maana upatanisho ni ahera.By kechi kenyatta / expired giant
Does this poem Deserve a thumbs up?
Yes

Download


Prev : Curved Destiny Next : Price Of FreedomSharing is Caring


Comments

 • Alice
  Heko
  352 wk ago
 • Chris
  Heko ndugu, si wengi wana uwezo wa kutungu ushairi kwa lugha ya Kiswahili. Mimi mmoja wao, mpenzi wa Kiswahili lakini naipa Kiingereza kipaumbele.
  352 wk ago
 • Isabella Nkirote
  Hata komenti ni ngori kudosi Kechi
  352 wk ago
 • Shiruha Victor
  Eeeee kweli mwenzetu karogwa na penzi. Swadakta!!!!!!!!
  352 wk ago
 • Rick Okinda
  ustadi wako ni wa kusisimua, una uwezo mkubwa was kuwa guru katika fani ya kuwa malenga, Nazi pevu mno bwana
  351 wk ago
 • Rapando Jnr
  Heko ndugu
  351 wk ago
 • Kelvin Achuka
  Swadakta!!!hongera
  351 wk ago
 • Quin Bernards
  The only word nmeelewa ni penzi.. Nice piece of art though sijaelewa half of it coz oswayo ni taabu
  351 wk ago
 • Nannah
  hongera kaka.......
  350 wk ago
 • Didy
  Swahili is hard but that chiq is praised lol.good job
  349 wk ago

Fields marked with * are required